Leo tarehe 6/3/2024 Mhe. Dkt. Peya Mushelenga , Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Namibia ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia na kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania.