Tarehe 4 Mei 2026, nchini Namibia huadhimishwa Siku ya Mashujaa wa Ukombozi (Cassinga Day), ikiwa ni siku ya kitaifa ya kumbukumbu ya mashujaa waliopoteza maisha yao wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo, hususan kufuatia tukio la kihistoria la mashambulizi yaliyotokea katika eneo la Cassinga, kusini mwa Angola karibu na mpaka wa Namibia mwaka 1978.

Maadhimisho ya kitaifa mwaka huu yamefanyika katika mji wa Outapi, uliopo kaskazini mwa Namibia, yakilenga kuenzi historia ya mapambano ya ukombozi na kuthamini mchango wa waliotoa maisha yao katika harakati za kuikomboa nchi.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi -Ndaitwah, Rais wa Jamhuri ya Namibia.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa chama tawala cha SWAPO, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wapigania uhuru wa zamani, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, pamoja na wananchi wa kawaida.

Katika picha, kuanzia kushoto ni Mheshimiwa Balozi Caesar Chacha Waitara; Balozi wa Zimbabwe nchini Namibia; Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Biashara wa Namibia; pamoja na aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Namibia.