Tarehe 3 Mei 2026, Mheshimiwa Balozi Caesar Chacha Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia aliungana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Kaskazini mwa Namibia, katika mji wa Oshakati, Mkoa wa Oshana, kuadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanzania.
Katika sherehe hiyo, Mheshimiwa Balozi alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo nao, ambapo walijadili kwa kina masuala mbalimbali yahusuyo biashara, uwekezaji, pamoja na huduma za kikonseli.



