Tarehe 01Juni 2026, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia ulipokea ujumbe kutoka Benki ya CRDB ulioongozwa na Bi. Alfredina Kuzilwa kutoka Makao Makuu ya Beni hiyo kwa lengo la kujitambulisha rasmi na kufanya mazungumzo na uongozi wa Ubalozi kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Ubalozi, hususan katika kuimarisha ushirikano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Namibia.

Ujumbe huo ulikuwa nchini Namibia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Tatu wa uwekezaji na Biashara Barani Afrika, uliofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Mei 2026 katika jiji la Swakopmund, Namibia.