Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Namibia Hayati Dkt. Hage G. Geingob. Rais Samia alisaini kitabu hicho katika ofisi za Ubalozi huo Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2024.