Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia, tarehe 28 Novemba 2025 alitembelewa na Mhe. Mohamed B. Beigi, Balozi wa Iran nchini Namibia, katika ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha.
Katika mazungumzo yao, pande zote mbili zilijadili masuala mbalimbali yanayohusu uwakilishi wao nchini Namibia, pamoja na uhusiano baina ya Tanzania na Namibia.
