Tarehe 12 Februari 2026 Mhe. Balozi Caesar Waitara alipata fursa ya kutembelewa Ubalozini na Mheshimiwa Jacqueline N. Maongozi, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Ruvuma, ambaye yupo nchini Namibia kwa ajili ya kutafuta na kukuza fursa za biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Namibia.
