Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amejumuika na Jumuiya ya Watanzania waishio Kaskazini mwa Namibia kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Mhe. Balozi amewahakikishia Wanajumuiya ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.