Leo tarehe 7/5/2025, Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ametembelewa katika ofisi za Ubalozi na Mhe. Sam Shafiishuna Nujoma, Gavana wa Mkoa wa Khomas, jijini Windhoek, Namibia.
Lengo la kukutana lilikua ni kuangalia maeneo ambayo jiji la Windhoek linaweza kushirikiana na miji ya Dodoma na Zanzibar.
Ifahamike kuwa jiji la Windhoek ambalo lipo katika Mkoa wa Khomas ndiyo mji Mkuu wa Namibia na umepiga hatua katika maendeleo ya miundombinu na mipango miji ukilinganisha na miji mingine nchini Namibia.
Mazungumzo yao yalilenga katika kuanzisha mashirikiano ya kimiji kati ya jiji la Windhoek na miji ya Dodoma na Zanzibar.



