Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Caesar C. Waitara, amempokea Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima aliyewasili nchini humo leo tarehe 1 Septemba 2025, kushiriki Mkutano wa Wajane Afrika, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 3 - 5 Septemba 2025, jijini Windhoek.

Mhe. Dkt. Gwajima ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, ameambatana na Mhe. Mama Anna Mkapa pamoja na wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.