Leo tarehe 26 Februari, 2025 Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amempokea Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM ambaye amewasili nchini Namibia kuomboleza na wananchi wa Namibia kufuatia kifo cha Dkt. Sam Nujoma, Rais wa kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa la Namibia kilichotokea tarehe 8 Februari, 2025.
Balozi Dkt. Nchimbi atashiriki Memorial Service ya Mhe. Dkt. Nujoma ambayo itafanyika tarehe 28 Februari 2025 na atashiriki pia katika mazishi ya kiongozi huyo wa Namibia ambayo yatakayofanyika tarehe 1 Machi, 2025 katika makaburi ya Heroes Acre yaliyopo Windhoek-Namibia.
Ifahamike kuwa, mahusiano yaliyopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Tawala cha SWAPO cha Namibia ni ya muda mrefu na ya kihistoria.
