Mhe. Caesar Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na Mhe. Utoni Nujoma. Waziri wa Kazi, Mahusiano ya Viwanda na Ajira wa Namibia kwa lengo la kujitambulisha na kujadili maeneo ya mashirikiano katika masuala ya Ajira baina ya Tanzania na Namibia.