Leo tarehe 8 Novemba, 2023, Mhe. Caesar Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Namibia (NAMPORT) kwa lengo la kujitambulisha na kujadiliana masuala mbalimbali ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia hususan katika Sekta ya Bandari.


