Leo tarehe 12 Disemba, 2023, Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na Balozi Penda Naanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Namibia na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo kwa lengo la kujitambulisha na kujadili maeneo ya Ushirikiano.



