Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na Bw. Bornventura Mbidzo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Namibia kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumzia maeneo ya ushirikiano kati ya Bodi hiyo na Bodi ya Utalii ya Tanzania.