Leo tarehe 7 Novemba, 2023, Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na Mhe. Nevile Andre, Gavana wa Mkoa wa Erongo, nchini Namibia kwa lengo la kujitambulisha na kujadili namna ya kushirikiana kati ya Mkoa wa Erongo na Mikoa ya Dar, Manyara na Mwanza.


