Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek nchini Namibia leo tarehe 27 Februari 2025. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maombolezo ya Kitaifa na Ibada ya kumuaga aliyekuwa Rais wa kwanza wa Namibia Hayati Dkt. Sam Nujoma itakayofanyika tarehe 28 Februari 2025.