Mahafali ya kwanza ya wanafunzi 26 raia wa Namibia waliokuwa wakijifunza lugha ya Kiswahili kwa njia ya mtandaoni katika ngazi ya awali kwa muda wa wiki 15, yamehitimishwa tarehe 19 Novemba 2025 katika Chuo cha Triumphant kilichopo Windhoek, Namibia.

Mafunzo hayo yalidhaminiwa na Chuo cha Triumphant na yaliendeshwa na BAKITA.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia, ambaye katika hotuba yake aliwashukuru wanafunzi kwa kufanikisha kukamilisha mafunzo hayo. Aidha, aliwahamasisha kuendelea na mafunzo katika ngazi inayofuata.