Tarehe 19 Desemba 2025, Mheshimiwa Caesar C. Waitara, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, alipata fursa ya kutembelewa na Mheshimiwa Gabriel P. Sinimbo, Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania, katika ofisi yake jijini Windhoek, kwa lengo la kujitambulisha.
Mheshimiwa Balozi Sinimbo ni Balozi mpya nchini Tanzania, ambaye aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 11 Desemba 2025.
Katika mazungumzo yao, Mabalozi hao walijadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia

