Leo tarehe 24/03/2025 Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umepata fursa ya kutembelewa na Timu ya Makamanda kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania.

Timu hiyo imeongozwa na Kanali Lissu Njoghomi Murra, Kamanda wa Kitivo cha mafunzo kutoka Chuo cha Ukamandi na Unadhimu Tanzania. Makamanda hao watakua nchini Namibia kuanzia tarehe 24 hadi 29 Machi, 2025.

Ziara hii ni sehemu ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya kijeshi na imejumuisha Makamanda kutoka nchi za Burundi, DRC, Egypt, India, Kenya, Nigeria, Rwanda, Uganda, Zambia na Tanzania.