Leo tarehe 22 Aprili, 2025 ujumbe wa Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ukiongozwa na Col. Hamis Almas Lussuna, pamoja na Maj. Jela Joseph Bega na Maj. Biswaro Charles Malima kwa pamoja wamepata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia na kusalimiana na Mheshimiwa Caesar Chacha Waitara, Balozi waTanzania nchini Namibia.

Ujumbe huo utakuwepo nchini Namibia kuanzia tarehe 20 hadi 26 Aprili 2025 kwa ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na Chuo kikuu cha Namibia Kitivo cha Sayansi ya Kijeshi.

Ifahamike kuwa,  uhusiano wa Kijeshi kati ya Namibia na Tanzania ni wa muda mrefu na yenye manufaa kwa nchi zote mbili.