Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia tarehe 2 Septemba 2025 umepata heshima ya kutembelewa na Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake  na Wenye Mahitaji Maalum pamoja na Mhe. Mama Anna Mkapa, Mwenza wa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania wakiwa wameambatana na maafisa mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Lengo la ujumbe huo kutembelea Ubalozi ilikuwa ni kusalimia na kupata maelezo mafupi kuhusu utendaji kazi wa Ubalozi kutoka kwa Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia.

Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea jengo la Ubalozi ambalo limenunuliwa na kumilikiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.