Leo tarehe 24 Aprili 2025, Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Frans Kapofi (Mb), Waziri wa Ulinzi na Masuala ya Wapigania Uhuru (Ministry of Defense and Veteran Affairs) wa Namibia katika Ofisi ya Wizara hiyo.

Lengo la mkutano huo ilikuwa ni;

Moja, kumpa hongera Mhe. Kapofi kwa kuaminiwa na kuteuliwa tena na Mamlaka kushika nafasi hiyo.

Pili, kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Ulinzi kati ya Tanzania na Namibia ambapo pande zote mbili zilikubaliana umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo.