Leo, Mhe Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia alipata heshima ya kushiriki katika mahafali ya kundi la pili la wanafunzi wa Kswahili katika Chuo cha Triumphant College, Namibia, ambapo jumla ya wanafunzi 37 wamehitimu.

Ni hatua muhimu ya maendeleo ya Kiswahili nchini Namibia. Muda kama huu mwaka jana, wanafunzi 26 walihitimu katika kundi la kwanza. Kuongezeka kwa idadi hiyo hadi 37 mwaka huu ni ishara ya kukua kwa hamasa na mwitikio wa kujifunza Kiswahili.

Mgeni Rasmi, Balozi Humphrey Geiseb, alimwakilisha Mhe. Selma Ashipala-Musavyi, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Biashara wa Namibia.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa alisisitiza kuwa Kiswahili si Lugha tu, bali ni daraja la kuunganisha watu, kuimarisha diplomasia, kukuza biashara na utalii, pamoja na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia.

Hongereni wahitimu wote 37!

Kiswahili ni fahari yetu, utambulisho wetu na daraja la kuunganisha Afrika. Tukienzi, tukikuze na tukivushe mipaka!