Leo, tarehe 11 Novemba 2026, Mheshimiwa Denis Lazaro Londo (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashar,a akiwa ameambatana na ujumbe wa wataalamu kutoka Tanzania, ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, jijini Windhoek, na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Caesar C. Waitara, pamoja na watumishi wa Ubalozi.
Mhe. Naibu Waziri yupo nchini Namibia kushiriki Kikao cha Pamoja cha mwaka 2026 cha Kamati ya Kiserikali ya Maofisa Waandamizi na Wataalamu wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini (ICSOE), kinachofanyika tarehe 10 - 13 Novemba 2026.

