Leo, tarehe 11 Julai 2026, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia unadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali katika kusherehekea lugha ya Kiswahili na mchango wake katika kuimarisha umoja, utamaduni, elimu, biashara, diplomasia na ushirikiano barani Afrika.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mheshimiwa Jennely Matundu, Naibu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Biashara wa Jamhuri ya Namibia.
Miongoni mwa Mabalozi wa nchi nyingine waliohudhuria Maadhimisho hayo ni pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Angola na Zimbabwe.
Katika maadhimisho hayo, wageni wamepata fursa ya kutembelea maonesho ya vitabu vya Kiswahili, bidhaa mbalimbali za Tanzania pamoja na kazi za ubunifu zinazoakisi urithi, utamaduni na utajiri wa Tanzania





















