Kwa ubalozi wa Tanzania nchini Namibia, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili 2026 hayakuwa tu sherehe ya lugha, bali pia jukwaa la kuitangaza Tanzania kupitia bidhaa zake mbalimbali.

Kuanzia vyakula, viungo hadi bidhaa za asili, kila bidhaa iliakisi ubora, urithi wa kitamaduni na utajiri wa Tanzania, huku ikiwapa wageni fursa ya kuonja na kujionea ladha halisi ya Tanzania.