Mhe. Balozi Ceasar Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ametembelewa na Prof. Osmund D. Mwandemele, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Utawala (International University of Management -IUM) nchini Namibia. Prof Mwandemele ni Mtanzania na ameishi Namibia kwa miaka 33.