Leo tarehe 28 Februari, 2025. Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umepata fursa ya kutembelewa na Mhe. Dennis Londo (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ( Anayesimamia masuala ya EAC).

Mhe. Londo alipokelewa na mwenyeji wake Mhe. Caesar Waitara, Balozi wa Tanzania Nchini Namibia pamoja na watumishi wa Ubalozi ambapo alipata fursa ya kukagua jengo na mazingira ya Ubalozi.

Mhe. Naibu Waziri ameambatana na Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania ambaye yupo nchini Namibia kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya kitaifa ya kumuaga Mhe. Dkt. Sam Nujoma, Rais wa kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa la Namibia ambayo itafanyika tarehe 28 Februari, 2025 jijini Windhoek.