Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umepata wasaa wa kutembelewa na ujumbe kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Tanzania (HESLB) ambayo ipo katika ziara ya kikazi nchini Namibia.
Lengo la ziara hiyo ni kuangalia namna ya kuboresha mfumo wa sasa wa ugharimiaji elimu ya juu. Ujumbe wa HESLB unakutana na taasisi mbalimbali ukiwemo Mfuko wa kuwezesha Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Namibia (NSFAF)
Ujumbe huo umeongozwa na Prof. Joel Mtebe ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB.


