Leo tarehe 28 Februari, 2025 Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ameambatana na Mwenza wake Bibi. Mbonimpaye Mpango kushiriki katika shughuli ya kitaifa ya kumuaga Mhe. Dkt. Sam Nujoma, Rais wa kwanza wa Namibia na Baba wa Taifa wa Namibia ambayo amefanyika leo tarehe 28 Februari, 2025 kwenye Uwanja wa Uhuru wa jijini Windhoek.

Mhe. Makamu wa Rais ameongoza ujumbe wa Tanzania katika shughuli hiyo ambapo amemuwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mazishi rasmi ya Dkt. Nujoma yatafanyika tarehe 1 Machi, 2025 katika Makaburi ya Mashujaa (Heroes' Acres) yaliyoko Jijini Windhoek, Namibia.