Leo tarehe 27 Juni 2024 Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amefanya mahojiano ya uzinduzi rasmi wa kuionesha Royal Tour Film kupitia Television ya Taifa ya Namibia Broadcasting Corporation (nbc) ambayo itarushwa mara 8 kila mwezi kwa muda wa miezi 7 kupitia chaneli ya “EYE on SADC" ya Television hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi za nbc.

Aidha ifahamike kuwa chaneli hiyo sio tu inaonekana nchini Namibia bali pia katika nchi zote ambazo ni wanachama wa SADC. Hivyo, itapelekea filamu hiyo kuonekana na wadau wengi ndani ya nchi hizo ambapo itaongeza hamasa ya watalii wengi kutaka kutembelea Tanzania.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia na Namibia Broadcasting Corporation.