Leo tarehe 7/3/2024 Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia umetembelewa na Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kwa lengo la kushiriki ufunguzi wa Mpango wa Hiari wa Afrika wa Kujitathimini katika Masuala ya Demokrasia na Utawala Bora (APRM) uliofanyika Ikulu ya Namibia.



