Leo tarehe 1 Agosti, 2024, Ubalozi umetembelewa na Dkt. Susan A. Kolimba aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amewasili nchini Namibia kushiriki Mkutano wa Kimkakati wa Kamati Tendaji ya Pan-African Women Organization - PAWO na Madhimisho ya miaka 62 ya PAWO, Dkt. Kolimba kwa sasa ni Katibu Mtendaji wa PAWO anayewakilisha Kanda ya Afrika Mashariki. Namibia ni mwenyeji wa mkutano huo ambao utafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 3 Agosti, 2024.